Tuesday, 6 September 2016

Nimelewa

Au labda niko tipsy kidogo,
..nimeonja whisky, si uongo,
sijui ati tot, tule tuglass tudogo,
Nimekunywa mbili, na nkaongeza kidogo,
..sai nafeel, vifunny kwa ubongo..
As if nafikiria na kisogo..
..but ukweli nikuwa we ndo wangu wa roho..
..Niamini juu, ni mlevi na mtoto tu ndo husema ukweli..

Hakuna anayejua kilicho moyoni,
..but walidai ati Love is blind, na mimi sioni,
nikiishi bila wewe, either leo au siku za usoni..
juu uko mrembo kwanzia Rohoni hadi usoni..
..Niamini juu, ni mlevi na mtoto tu ndo husema ukweli..

Ikifika kwako, Nitastaga kimwendo lakini sio kimawazo,
Wewe ndo sababu yangu ya kulewa mwanzo,
..juu nimeshindwa kukutoa kwenye mawazo,
,yangu...
Kama land lord na end month,
..au socialite amekosa ule mgeni end month,
....Niamini, juu ni mlevi na mtoto tu ndo husema ukweli...

Walai, nikona Makaa na sufuri, e.t.c
,jiko tu ndo sina..
..na mum aliniambia anatamani kuona moto yenye nitaasha,
....if moshi itajaa kwa nyumba..
..na kwa soko wewe ndo jiko ninayotamani,
Niliyoenzi, tangu zamani..
...itabidi umeniwia radhii samahani,
Na uniiamini tu juu, ni mlevi na mtoto tu ndo husema ukweli..

As I said,
Ni tot mbili tu,
...zinafanya niseme izi vitu..
What if ningepewa zaidi ya tatu..
..am sure ungetoka kwa pango,
...na uingie kwenyu mpango,
wangu, wa maisha..
juu kama kukupenda ni hatia,
me nikitayari kufunguwa pingu za maisha,
,na wewe..
Kwani wewe ndiye wa kiwewe..
..Niamini juu, ni mlevi na mtoto tu ndo husema ukweli..

Itabidi umeamini..
..kwani mimi ninaimani,
,kuwa Mungu alikuleta kwangu kimaksudi,
...kwangu najua utashika kama colour ya msudi,
kama kikupenda ni makosa, nitatenda bila kusudi,
,,eyes on the price, nyuma sirudi...
..Niamini juu, ni mlevi na mtoto tu ndo husema ukweli..

mimi kama mlevi nasema ukweli,
..nakupenda, ile cha ukweli,
am drunk in love...
Na wewe ndo mgema..
So please usitilie maji,
Juu nitakusifu kwa wenzangu,
..vile nimelewa mara mbili,
..Na wataniamini tu juu, ni mlevi na mtoto tu ndo husema ukweli..

                         ⓒ2016

No comments:

Post a Comment